Malalamiko ya jinai yanasema kuwa vitendo vya Kadosh vilichochewa na tofauti za kidini na kikaumu. Kadosh alidaiwa kutishia kuingia katika nyumba ya Chebira na kumuua kwa sababu ya imani zao tofauti.
Alikamatwa siku ya Jumamosi, siku mbili baada ya kuripotiwa kuvunja nyumba ya Chebira, kuiharibu, na kuivunjia heshima Qur’ani Tukufu.
Siku hiyo hiyo, Kadosh alidaiwa kumpiga Chebira kichwani na panga na kumsababishia majeraha makubwa yaliyohitaji kulazwa hospitalini.
Chebira, ambaye alihamia katika jengo hilo mnamo Oktoba, aliripoti kuwa unyanyasaji huo ulianza muda mfupi baada ya kuwasili kwake. Alieleza kufarijika kwa kukamatwa kwa Kadosh, akihofia mashambulizi zaidi baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini.
3489525
Malalamiko hayo yanaelezea matukio ya mwanzoni mwa Machi, ikiwa ni pamoja na kukatwa kwa matairi, uharibifu wa milango, kushambuliwa kimwili na vitisho vya mara kwa mara kwa maisha ya Chebira.
Kumekuwa na hali tete katika visa vya chuki dhidi ya Uislamu kote Marekani na nchi nyingine kadhaa za Ulaya Oktoba mwaka jana wakati utawala katili wa Israel ulipoanzisha vita vya mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza.
3489525